Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imesema imetumia zaidi ya Sh milioni 120 kuboresha sekta ya mawasiliano katika Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Imesema fedha hizo zinatumika katika kuwezesha mawasiliano na machapisho mbalimbali katika maonesho hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Tuzo ya udhamini wa maonyesho hayo, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema kuwa fedha hizo zinatumika katika kuzalisha machapisho na mawasiliano kwa vyombo vya habari katika maonesho hayo.
“Tunatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kutangaza Maonesho haya ya Kimataifa ya Sabasaba kwani yanakusanya watu wengi kutoka sehemu mbalimbali na vyombo vya habari vinao mchango mkubwa katika kutoa taarifa kwa Watanzania ndio maana tumeamua kuwekeza kiasi hiki cha pesa katika kuhakikisha masuala yote ya mawasiliano yanafanyika vizuri ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa katika maonyesho haya,” alisema Kelvin .
Maonesho ya Sabasaba yanayodumu kwa siku 10, hukusanya watazamaji zaidi ya 350,000 na kutoa fursa kwa watazamaji kulinganisha ubora wa bidhaa na kufanya ununuzi.
0 comments:
Post a Comment